| Mwasika afungiwa mwaka mmoja! | |
|
|
Vurugu hizo ambazo hazitegemewi kutokea kwa wachezaji wanaojiita wa kulipwa zilihusisha baadhi ya wachezaji wa Yanga ambao walimvamia refarii wa mchezo huo Israel Mujuni. Wachezaji waliofungiwa ni Stephano Mwasika (mwaka mmoja), Nadir Haroub na Jery Tegete (mechi 6 kila mmoja), Nurdin Bakari na Omega Seme (mechi 3 kila mmoja). Kwa upande mwingine klabu ya Yanga imepigwa faini ya shilingi milioni 4.5. Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Yanga kuchapwa na Azam goli 3-1 mwamuzi alimtoa Haruna Niyonzima katika dakika ya 13 kwa kadi nyekundu kutokana na kuzozana na mwamuzi na kumtolea lugha chafu.
Mbali na mwamuzi kupigwa mali mbalimbali za uwanja huo ziliharibiwa ikiwa ni pamoja na viti ambavyo vilikuwa vikirushwa uwanjani na mashabiki wa Yanga. Yanga sasa itatakiwa kulipia uharibifu huo wa mali za uwanja kama wapinzani wao Simba walivyolipa milioni 5 baada ya mashabiki kuvunja viti katika mechi ya kombe la shirikisho waliyocheza na Kiyovu. TFF imetumia kanuni ya 25 ambayo inaelezea udhibiti wa wachezaji uwanjani. Katika kipengele (F) kifungu cha (ii) kinaeleza bayana kuwa mchezaji yeyote atakayemshambulia mwamuzi au kiongozi yeyote kwa namna yoyote ile, iwe kwa matusi au kwa kumgusa, ataadhibiwa kwa kufungiwa kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu hadi 12, kufungiwa kucheza michezo kadhaa, kupigwa faini kwa mujibu wa Kanuni ya 31 au vyote kwa pamoja. |
Kutokana na vurugu zilizotokea katika mechi ya Yanga dhidi ya Azam uwanja wa Taifa, kamati ya mashindano ya TFF imewafungia baadhi ya wachezaji wa Yanga na klabu kutakiwa kulipa faini.

Maoni
2012-03-1301:28:14 Hiyo sasa ndiyo fundisho kwa wachezaji wa bongo manake wamezidi kutudanganya ooohh sisi maprofeshno..kiko wapi sasa
2012-03-1414:53:27 Kweli hii ni aibu sana lini watanzania tutaendelea. Mchezaji unawezaje kumfukuza refarii na polisi hawafanyi chechote kile.
2012-03-1701:31:40 Hivi ndio mnategemea watu watapenda mpira wa kitanzania?kwanza hauna mafanikio,pili hauna mvuto zaidi ya majigambo na mwisho wachezaji hawana nidhamu.Tunawasubilli nao waanze tabia za usagaji kama mastaa wa uigizaji wanavyofanya
2012-03-1811:53:38 Sawa tumeona hayo yametokea! Lakini wapunguziwe adhabu .
2012-03-2411:15:52 hivyo ni baadhi ya vitu ambavyo daima vitachelewesha maendeleo ya soka hapa nchini. wachezaji na washabiki tuheshimu sheria za michezo.