| Arsenal Vs Newcastle United | |
|
|
Arsenal wakishinda mchezo huu watakuwa wamefikisha idadi ya michezo mitano ya ushindi mfululizo kwenye mashindano hayo ya ligi kuu kwani hapo awali walishinda dhidi ya Liverpool (2-1), Tottenham (5-2), Sunderland (2-1) na Blackburn (7-1). Wachezaji wake waliokuwa majeruhi Mikel Arteta (aliyeumia kichwa) na Aaron Ramsey (enka) wote wana uhakika wa kurejea leo. Pia wamo Yossi Benayoun na Andre Santos. Hata hivyo wachezaji wanaorejea kutoka majeruhi wanaweza wasianzishwe katika kikosi cha kwanza hasa kutokana na kiwango kizuri kilichoonyeshwa na Oxlade-Chamberlain na Tomas Rosicky katika mechi dhidi ya AC Milan waliposhinda 3-0. Arsenal waliopoteza nafasi ya kucheza UEFA watakuwa na kazi ya kushinda leo ili wajiweke katika nafasi nzuri ya kushiriki micuano hiyo tena mwakani hasa kutokana na ushindani uliopo katika nafasi ya nne kati yao, Chelsea, Newcastle na Liverpool. Lakini itakuwa sio kazi rahisi kwa Arsenal kushinda mbele ya Newcastle united ambao mpaka sasa hawajashinda hata mchezo mmoja katika michezo mitatu waliyocheza kwa kutoka sare ya 1-1 walipowakaribisha Sundeland, sare ya 2-2 nyumbani kwao na Wolves, kufungwa 5-0 ugenini walipocheza na Tottenham. Shola Ameobi anaweza kurejea leo kuichezea Newcastle lakini majeruhi wengine kama Peter Lovenkrands, Sammy Ameobi, Leon Best na Steven Taylor. Kwa upande wa piga nikupige Newcstle wanaweza kusimamia hadi kucha kama walivyofanya msimu uliopita walikuwa nyuma kwa magoli 4-0 na wakamudu kusawazisha yote ndani ya dakika 19 za mwisho za mchezo na bado wakawa wanawawinda kupata la ushindi. Katika mechi ya awali msimu huu Arsenal waliposafiri hadi Newcastle, timu hizo zilitoka 0-0 huku mchezaji wa arsenal, Gervinho, akipewa kadi nyekundu. DONDOO MUHIMU KABLA YA MECHI YA LEO :: Arsenal watacheza mchezo wa leo wakiwa wamewazidi Newcastle kwa pointi 5 :: Arsenal wakishinda watakuwa ponti 1 tu nyuma ya Tottenham walio nafasi ya nne na hivyo kuzidi kujihakikishia nafasi nzuri mwisho mwa msimu :: Arsenal ameshindwa kushinda dhidi ya Newcastle katika mechi tatu za ligi kuu walizokutana na ushindi wao wa mwisho ulikuwa mwaka Machi 2009 :: Arsenal wanajivunia mfungani wao hatari Robin Van Persie mwenye magoli 25 wakati wapinzani wao wanaye Demba Ba mwenye magoli 16 :: Katika mechi tatu za mwisho walizokutana, Arsenal ilijikuta ikipoteza mchezaji mmoja kwa kadi nyekundu Gervinho, Abou Diaby and Laurent Koscielny. |
Timu ya Arsenal leo usiku inawakaribisha Newcastle United katika uwanja wa Emirates katika moja ya mechi za ligi kuu Uingereza.
