Sunday 05th of September 2010

Home
Habari za Michezo
Capello kutompanga Rooney
Monday, 30 August 2010 05:44

LONDON, England
  
KOCHA wa timu ya soka ya Taifa ya England, Fabio Capello ameonesha kuwa hatampanga Wayne Rooney katika kikikosi kitakachoanza mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Ulaya dhidi ya Bulgaria.

Mshambuliaji huyo nyota, Rooney hajaanza msimu mpya vizuri na hakusafiri na timu yake ya Manchester United ilipocheza na Fulham siku sita zilizopita kutokana na maumivu ya tumbo. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2.

Kocha Capello atamuanzisha  Rooney katika kikosi chake kwenye Uwanja wa  Wembley, Ijumaa iwapo atakuwa fiti kwa mechi hiyo.

Read more...
 
Ferguson amshukia Wenger
Monday, 30 August 2010 05:42

MANCHESTER, England
 
KOCHA wa Manchester United, Alex Ferguson amemwambia wa Arsenal, Arsene Wenge kuwa atoe boriti kwenye jicho lake kabla hajaona kibanzi kwenye jicho la mwenzake,

Ferguson amempasha Wenger kuwa ni vyema akaangalia kwanza mambo ya timu yake kabla ya kumshambulia Paul Scholes wa United, juu ya ubaya wake.

Kocha huyo wa Manchester United alieleza kushangazwa kwake na tuhuma za Mfaransa huyo na yeye angeweza kusema kama hayo kwa mchezaji mmoja wa Arsenal, lakini hataki kufanya hivyo.

Read more...
 
Yanga bingwa - Nahodha
Thursday, 26 August 2010 05:41

Na Laurent Samatta
MSHAMBULIAJI wa timu ya Yanga, Abdi Kassim, amesema kuwa huu ni msimu wao wa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu.

Kassim ambaye mara kadhaa anavaa beji ya unahodha wa Yanga alisema kuwa dalili hizo zinatokana na kushinda mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya bingwa mtetezi, Simba.

Katika ufunguzi wa Ligi Kuu, timu ya Yanga iliichapa Polisi Dodoma 1-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma na kuana vizuri kampeni za kulitafuta taji linaloshirikiliwa na Simba.

Kassim alisema jana kuwa wana hakika msimu huu taji lazima walichukue kutokana na malengo madhubuti waliojiwekea ambayo ndiyo silaha kubwa ya wao kulibeba kombe hilo linalopinganiwa na timu 12.

Read more...
 
Yanga bingwa
Thursday, 26 August 2010 05:50

 

 
Ngassa, Mgosi waandalia kuiua Algeria
Thursday, 26 August 2010 05:40

Na Erasto Stanslaus

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Jan Paulsen amewapa mazoezi maalum washambuliaji wake kwa ajili ya kuimaliza timu ya Algeria katika mchezo wao.

Stars itavaana na Algeria Septemba 3 wakiwa ugenini, katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwaka 2012.

Mchezo huo utakuwa wa pili kwa Mdenimaki huyo baada ya ule dhidi ya Kenya wa kirafiki uliomalizika kwa sare ya 1-1 na kumpa mwanga kwa kukiandaa kikosi hicho.

Read more...
 
« StartPrev12345678910NextEnd »

Page 2 of 52

Swali la Leo

"Kitendo cha mabondia wa ngumi za ridhaa kususia mashindano kutokana na kutopatiwa chakura na nauli, ni maamuzi sahihi kwa maslahi ya Taifa letu?"
 

Who's Online

We have 5 guests online

Login Form




Powered by Business Times Ltd Valid XHTML and CSS.