Sunday 05th of September 2010
Home
Habari za Michezo
|
Phiri arejesha amani Simba |
|
Sunday, 01 August 2010 10:00 |
|
Na Chausiku Omary

PAMOJA na kuchelewa kuripoti kwa Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri baadhi ya wanachama wa klabu hiyo wamesema kurejea kwake kumewapa matumaini ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu Bara msimu ujao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanachama hao walisema, Kocha huyo kwa kushirikiana na kocha msaidizi Amri Saidi kwa kiasi kikubwa msimu uliopita waliifikisha mbali timu hiyo hivyo kurejea kwake kunawapa matumaini ya kuendeleza ubingwa wa mara ya pili.
|
|
Read more...
|
|
|
Saturday, 24 July 2010 15:51 |
|
Jeshi la Yanga hatari Na Julius Kihampa KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Kostadin Papic ametangaza jeshi lake la askari 27 litakalopigania ubingwa wa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara. Jeshi hilo litakuwa na kazi ngumu ya kuhakikisha wanarudisha taji lao la ubingwa walilopokwa msimu uliopita na watani wao wa jadi, Simba. Msemaji wa klabu hiyo, Louis Sendeu alisema wamesajili wachezaji 27 ambao walikuwa wakitakiwa na kocha wao mara baada ya kumaliza kwa msimu uliopita. Kwa idadi hiyo ya wachezaji Yanga imewazidi wapinzani wake wa jadi, Simba kwa mchezaji mmoja kwani wao wamesajili wachezaji 26.
|
|
Read more...
|
|
?Mtoto wa Papic aiua Simba SC |
|
Saturday, 24 July 2010 15:49 |
|
Na Mohamed Akida UJIO wa mtoto wa Kocha Mkuu wa Yanga, Kostadin Papic, Todor umeongeza hali ya ushindi kwa timu ya Yanga dhidi ya Simba kutokana na mtoto huyo kumshinikiza baba yake kushinda mechi hiyo. Yanga itavaana na Simba, Agosti 14 katika mchezo wa Ngao ya Jamii kabla ya kuanza kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara utakaoanza Agosti 21. Todor aliliambia Spoti Starehe, juzi mazoezini kuwa furaha yake ni kuona Simba inafungwa na hilo anaamini litafanikiwa kutokana na baba yake kujua mapenzi yake yapo wapi. “Baba anajua ni jinsi gani nisivyoipenda rangi nyekundu na nashukuru baba anafundisha timu yenye rangi za njano na kijani,” alisema Todor.
|
|
Read more...
|
|
|
Saturday, 24 July 2010 15:50 |
|
Na Chausiku Omary MANENO aliyoyatoa Kocha Msaidizi wa Simba, Syllersaid Mziray ni ishara tosha kuwa amewamaliza kabisa watani wao jadi, Yanga. Mziray ameanza kuifundisha Simba, mwanzoni mwa wiki hii na tayari ametoa kauli kali kwa watani wao wa jadi watakaokutana nao Agosti 14 katika mchezo wa Ngao ya Jamii. Kocha huyo mkongwe katika medani ya soka nchini amesema kwa kikosi alichokikuta Simba, Yanga wataumia watake wasitake. “Kwa kikosi hiki, Yanga waandike wameumia kwani sidhani kama watapata ushindi katika michezo yote mitatu, tutakayokutana nayo msimu ujao,” alisema Mziray. Mziray ambaye ni mtaalamu wa viungo aliongeza: “Nina wiki moja na timu lakini kabla kukutana na Yanga, kikosi changu kitakuwa kinatisha sana, nawaonea huruma watani wetu wa jadi kukutana nao Agosti 14”.
|
|
Read more...
|
|
?Joto la Simba, Yanga laanza kupanda |
|
Saturday, 24 July 2010 15:45 |
|
Na Chausiku Omary JOTO la mchezo wa watani wa jadi wa Simba na Yanga limeanza kupanda baada ya wachezaji wa timu hizo kuanza kutambiana kuibuka na ushindi. Miamba hiyo itakutana katika mchezo wa kwanza wa Ngao ya Jamii utakaopigwa Agosti 14 ikiwa ni ufunguzi wa pazia la msimu wa Ligi Kuu Bara utakaoanza Agosti 21. Simba na Yanga watakutana tena katika mchezo wa kwanza wa ligi hiyo katika mzunguko wa kwanza Oktoba 16. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachezaji nyota wa timu hizo wameanza tambo kwa kila mmoja akimtambia mwenzie kuwa ataibuka na ushindi katika mchezo huo.
|
|
Read more...
|
|
|
|
|
|
|
Page 10 of 52 |
Who's Online
We have 6 guests online
Powered by Business Times Ltd
Valid XHTML and CSS.