Sunday 05th of September 2010

Home
Habari za Michezo
Simba, Yanga sasa Agosti 18
Wednesday, 04 August 2010 05:52

* Wamisri waitosa Stars, waangukia kwa Kenya

Na Erasto Stanslaus

KAMBI ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imesababisha kusogezwa mbele kwa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga, uliokuwa ichezwe Agosti 14 sasa utapigwa Agosti 18.

Stars inatarajia kuingia kambini leo kujiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Kenya utakaopigwa Agosti 11, ambao awali ulikuwa uchezwe na Misri mjini Cairo.

Katika kikosi hicho timu ya Yanga inawachezaji nane wakati wapinzani wao Simba inawachezaji saba.

Read more...
 
Paulsen awarudisha Chuji, Kaseja Stars
Wednesday, 04 August 2010 05:48

* Boban avutiwa pumzi

Na Erasto Stanslaus

KOCHA mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Jan Paulsen jana alitangaza kikosi chake cha kwanza kitakachoivaa timu ya Misri kikiwa na wachezaji walitemwa katika kikosi hicho na Marcio Maximo, Juma Kaseja na Athumani Idd 'Chuji'.

Kaseja, Chuji, Haruna Moshi 'Boban' na Amir Maftah walitimuliwa kwa nyakati tofauti na Maximo kwa madai ya utovu wa nidhamu na hakuwaita tena katika kikosi hicho.

Kikosi kilichotajwa na Paulsen jana kinajiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Misri utakochezwa Agosti 11, ikiwa ni maandalizi ya kuwania tiketi ya kufuzu fainali za Afrika.

Akitangaza lengo la kuwarudisha nyota hao, Paulsen alisema baada ya kuja ameelezwa kuwa wachezaji hao wana uwezo lakini walienguliwa katika kikosi hicho kutokana na utovu wa nidhamu, hivyo ameamua kuwarudisha ili ajionee mwenyewe.

Read more...
 
Mgosi: Lazima niifunge Yanga
Sunday, 01 August 2010 10:10

Na Laurent Samatta

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mussa Hassan 'Mgosi' amewachimba mkwara watani wao wa jadi, Yanga, kuwa lazima awafunge katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Agsoti 14.

Akizungumza na Spoti Starehe, Mgosi alisema Yanga wasahau kutwaa ubingwa kwani, taji hilo hawana mpango wa kuliachia.

Read more...
 
Simba full nondo
Sunday, 01 August 2010 10:11

Na Erasto Stanslaus

SIMBA sasa ni full nondo! Huo ndio usemi ambao unaweza kuusema baada ya kurejea Kocha Mkuu wa timu hiyo ambaye ameipa mafanikio makubwa katika msimu uliopita, si mwingine bali ni Patrick Phiri.

Kurejea kwa kocha huyo mwenye imani ya kilokole ambaye tayari alikuwa njia panda kutemwa na klabu hiyo baada ya kutafutiwa mrithi wake, ujio wake umepokelewa kwa shangwe na wachezaji wa timu hiyo.

Read more...
 
Papic kupata wa kuiua Simba
Sunday, 01 August 2010 10:09

Na Erasto Stanslaus

VITA kali itaonekana leo katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, wakati wachezaji wa Yanga watakapoonesha uwezo wa kumshawishi kocha wao, Kostadin Papic kuwa katika kikosi chake cha kwanza.

Papic amenadi kuwa tayari ana vikosi viwili ambavyo vyote vya kuotea mbali, lakini lazima awe na kimoja ambacho kitakuwa na kazi ya kwanza ya kuiua Simba Agosti 14.

Read more...
 
« StartPrev12345678910NextEnd »

Page 9 of 52

Swali la Leo

"Kitendo cha mabondia wa ngumi za ridhaa kususia mashindano kutokana na kutopatiwa chakura na nauli, ni maamuzi sahihi kwa maslahi ya Taifa letu?"
 

Who's Online

We have 5 guests online

Login Form




Powered by Business Times Ltd Valid XHTML and CSS.