Sunday 05th of September 2010
Home
Habari za Michezo
|
?Uchaguzi TASWA Agosti 14 |
|
Thursday, 05 August 2010 04:32 |
|
Na Shufaa Lyimo
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu Agosti 14 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Msaidizi wa chama hicho, Amir Mhando alisema awali uchaguzi huo ulipangwa ufanyike keshokutwa lakini umesogeza mbele kutokana na kupokea maombi kutoka kwa wanachama wao.
Mhando alisema mwisho wa kulipia kadi ni leo na kudai kuwa kila atakayeilipia kadi yake atapatiwa risiti ikiwa pamoja na kuchagua watu watakaosimamia uchaguzi huo na kuhakikisha unafanyika kwa haki.
|
|
Read more...
|
|
|
Thursday, 05 August 2010 04:30 |
|
Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa viungo wa timu ya Simba, Syllersaid Mziray amewabeza Yanga kuwa pamoja na kushinda ushindi mnono katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Telecom ya Mawali lakini timu hiyo bado sana.
Mziray ambaye alisafiri kutoka Zanzibar hadi Dar kwa lengo la kushudia mchezo huo ambao Yanga walishinda mabao 4-1, kitu ambacho kocha huyo mkongwe hakukubaliana nacho.
Kocha huyo aliyekuwa anakaimu nafasi ya Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri alisema Yanga ni wazuri katika kiungo na ushambuliaji lakini hawana ulinzi wa kuwazuia Simba.
|
|
Read more...
|
|
?Yossi ni zaidi ya Cole - Ancelotti |
|
Thursday, 05 August 2010 04:28 |
|
LONDON, England BAADA ya kumsota winga wake Joe Cole, Kocha wa timu ya Chelsea, Carlo Ancelotti ameweka wazi kuwa winga huyo alikuwa hafuati maagizo yake. Cole ambaye amejiunga na Liverpool baada ya kumaliza mkataba wake katika majira ya joto, lakini Ancelotti amemsajili Yossi Benayoun, ambaye anaamini ni bora kuliko Cole. Meneja huyo wa Stamford Bridge anasema: "Joe Cole anaspidi kuliko Benayoun lakini Yossi ni mzuri katika ufundi. Anaelewa nini ninachomwabia.” "Cole na Benayoun ni wachezaji tofauti na kila mmoja ananafasi yake, lakini ninafuraha kuwa na Yossi katika kikosi changu." Benayoun, amesaini Chelsea kwa dau la pauni milioni 5.5 akitokea Liverpool, na ujio wake utaifanya Blues kufanya vizuri katika mchezo wa Jumapili wa Ngao ya Jamii dhidi ya Manchester United. Chelsea pia wiki hii wamemsajili nyota wa Brazil aliyeng'ara katika fainali za Kombe la Dunia, Ramires baada ya kukubali dau la pauni milioni 18.3 akitokea Benfica. |
|
|
Thursday, 05 August 2010 04:29 |
|
MANCHESTER, England MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Wayne Rooney ameanza mazoezi na wenzake kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Chelsea utakaopigwa Jumapili. Rooney amerudishwa katika kikosi hicho na kocha wake Sir Alex Ferguson ikiwa ni kama adhabu baada ya kulewa chakali na kuvuta sigara kwa fujo. Rooney, 24 atalazimika kuwepo katika kikosi kitakachoivaa Chelsea, hivyo kuvunja ofa yake aliyopewa na Ferguson ya kukaa nje kwa mwezi mmoja. Mchezaji mmoja wa United alisema Sir Alex anataka kumtumia Rooney katika mchezaji huyo ili kumrudisha katika kiwango chake baada ya kuponda raha kwa muda mrefu. Pia kiungo wa timu hiyo, Anderson, 22, naye ameanza mazoezi na wenzake baada ya kunusurika kifo katika ajali ya gari aliyopata akiwa Ureno. |
|
Mkali Phiri ndani ya hausi |
|
Wednesday, 04 August 2010 05:59 |
|

|
|
|
|
|
|
|
Page 8 of 52 |
Who's Online
We have 5 guests online
Powered by Business Times Ltd
Valid XHTML and CSS.