Sunday 05th of September 2010
Home
Habari za Michezo
|
Thursday, 05 August 2010 04:43 |
|
Na Mohamed Akida
WACHEZAJI wa kimataifa wa Yanga kutoka Ghana jana waliibeba timu hiyo baada ya kuingia na kubadilisha na kupata bao la ushindi katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mchezo huo ambao ni wa pili kwa Yanga ulichezwa katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam huku ukiwa maalumu kwa kujipima nguvu kwa timu hizo.
Mpira huo ambao haukuwa na ushindani mkubwa huku timu hizo zikishindwa kuonesha kandanda safi hadi mapumziko timu hizo zilikuwa sare ya mabao 1-1.
Kocha Mkuu wa Yanga, Kostadin Papic ambaye hakuwa na nyota wake nane waliokuwa katika timu ya Taifa, aliwaweka nje wachezaji wake Waghana lakini mambo yalivyokuwa magumu alilazimika kuwaingia na kubadilisha mchezo.
|
|
Read more...
|
|
|
?Simba yafanya mauaji Z'bar |
|
Thursday, 05 August 2010 04:42 |
|
Na Mwajuma Juma, Zanzibar SIMBA imefanya mauaji katika mechi yake ya pili ya kujipima nguvu kwa kuicharaza Ngome ya hapa mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Fuoni. Mabingwa hao wa soka wa Bara wanaojiandaa na Ligi Kuu waliotoka suluhu na Azam katika mechi yake ya kwanza Jumapili iliyopita, walitumia dakika 30 za mwisho kupata magoli hayo. Goli la kwanza la Simba lilifungwa na Patrick Ochan dakika ya 61 baada ya kuunganisha krosi ya Shija Mkina na Mganda huyo kufunga la pili dakika ya 75 kwa pasi ya Haruna Shamte.
|
|
Read more...
|
|
?Kado amchimba mkwara Kaseja |
|
Thursday, 05 August 2010 04:37 |
|
Na Addolph Bruno
KIPA wa Taifa Stars na Mtibwa Sugar, Shaabani Kado amesema atahakikisha haipotezi namba yake katika kikosi hicho pamoja na ujio wa Juma Kaseja.
Akizungumza Dar es Salaam juzi Kado alisema anamshukuru Jan Poulsen kumpa nafasi katika kikosi chake na kuongeza kuwa atatumia uwezo wake wote kuitumikia vizuri Taifa Stars.
"Nimeitwa katika kikosi cha Paulsen lakini naamini nitakutana na mtihani wa kupata namba mbele ya Kaseja, ila nimejipanga kuibakisha namba yangu kwa juhudi zote," alisema Kado.
|
|
Read more...
|
|
|
?Huu ni msimu wetu – Yanga |
|
Thursday, 05 August 2010 04:39 |
|
Na Shufaa Lyimo YANGA wamesema wana kila sababu ya kurudisha taji lao la ubingwa lililopokwa na mahasimu wao Simba katika msimu uliopita. Uongozi wa klabu ya Yanga umedai kuwa wamejipanga kuhakikisha hilo linafanikiwa kwa kutwa taji hilo mapema zaidi kutoka kwa Simba. Akizungumza Dar es Salaam jana, Afisa Habari wa klabu hiyo, Louis Sendeu alisema benchi la ufundi na uongozi mpya kila mmoja na nafasi wake wamekubaliana kurudisha taji hilo. “Mwalimu ameshatueleza kuwa yupo fiti kutwaa ubingwa wa msimu huu kutokana na usajili waliofanya ikiwa pamoja na maandalizi wanayoendelea nayo hadi sasa,” alisema Sendeu.
|
|
Read more...
|
|
Thursday, 05 August 2010 04:35 |
|
Na Zahoro Mlanzi
TIMU ya The Express ya Uganda, inatarajia kutua nchini kesho tayari kwa ajili ya kushiriki tamasha la Simba 'Simba day', litakalofanyika Jumapili Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Clifford Ndimbo alisema maandalizi ya tamasha hilo kwa kiasi kikubwa yamekamilika ambapo The Express itatua nchini kesho na msafara wa wachezaji 20 na viongozi watano.
Alisema timu hiyo itacheza na kikosi chote cha Simba ambacho siku hiyo kitatambulishwa rasmi kwa mashabiki wa timu hiyo ambapo pia itatoa fursa kwa Kocha Mkuu, Patrick Phiri kupata kikosi chake cha kwanza.
|
|
Read more...
|
|
|
|
|
|
|
Page 7 of 52 |
Who's Online
We have 4 guests online
Powered by Business Times Ltd
Valid XHTML and CSS.