Sunday 05th of September 2010
Home
Habari za Michezo
|
Monday, 16 August 2010 05:17 |
|
Na Shaban Mbegu
MIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, zinatarajiwa kumenyana Jumatano hii katika mechi ya Ngao ya Hisani ambayo ni ishara ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara msimu huu, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi hiyo, inatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wa timu zote hizo hasa kutokana na mechi hiyo kuwa ya kwanza huku kila upande ukitaka kuangalia usajili wake.
Mashabiki wa timu hizo watafurika uwanjani kujionea viwango vya wachezaji wapya wa timu hizo ambao wamesajiliwa kwa gharama kubwa na uongozi wa klabu zote kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje nchi.
Mchezo huu pia ndio utakaotoa dira ni kocha yupi amesajili wachezaji vizuri na ameiandaa vipi timu yake kwa ajili ya Ligi Kuu Bara msimu huu.
Mtanange huo ndio utakaotoa jibu ni mchezaji gani bora kati ya Keneth Asamoh raia wa Ghana aliyesajiliwa na Yanga na Patric Ochan wa Simba aliyetokea nchini Uganda.
|
|
Read more...
|
|
|
Manara atia mkono Simba, Yanga |
|
Monday, 16 August 2010 05:13 |
|
Na Mohamed Akida

WAKATI homa ya mpambano wa Ngao ya Jamii ikizidi kupanda kwa timu za Simba na Yanga, mchezaji wa zamani, Sunday Manara, amesema haipi nafasi timu yoyote kushinda mchezo huo kutokana na kanuni mbovu za kuendesha klabu hizo.
Manara ambaye aliwahi kuvuma akiwa na kikosi cha Yanga miaka ya nyuma, alisema anashindwa kuipa nafasi timu moja kati ya hizo kutokana na mfumo wao wa kuandaa timu na wachezaji kufanana na hivyo timu yoyote inaweza kushinda kwa sababu mchezo huo lazima mshindi apatikane.
"Timu yoyote inaweza kushinda kwa sababu lazima mshindi apatikane lakini timu hizo hazina wachezaji wenye malengo ni kama zimekusanya watu ilimradi wapate ushindi na sio ushindi ambao utatafutwa kwa maandalizi maalum kama ya kuwaandaa vijana wadogo kutoka katika timu zao za watoto," alisema.
|
|
Read more...
|
|
Simba, Yanga waonyeshana tambo |
|
Monday, 16 August 2010 05:12 |
|
Na Chausiku Omary
WAKATI vuguvugu la mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga likizidi kupamba moto uongozi wa klabu ya Simba umesema utapambana kufa au kupona ili kuhakikisha timu yao inaendelea kutetea taji la ubingwa.
Meneja Mkuu wa timu ya Simba, Innocent Njovu alisema hadi sasa kikosi chao kipo kamili na wanachosubiri ni siku ifike.
|
|
Read more...
|
|
|
Gumbo aichimba mkwara Yanga |
|
Monday, 16 August 2010 05:12 |
|
Na Andrew Ignas
MSHAMBULIAJI mpya wa Simba, Rashidi Gumbo, ametamba kukata ngebe za watani wao wa jadi, Yanga, kwenye mchezo wao wa Ngao ya Hisani unaotarajiwa kufanyika Jumatano Agosti 18, katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam saa 10 jioni. .
Mchezaji huyo alisema kuwa timu yake itaibuka kidedea kwenye mechi hiyo kwa kuwa wamefanya usajili mzuri na kupata mbinu nyingi kutoka kwa kocha wao, Mzambia Patrick Phiri.
"Yanga wajiandae kupokea kipigo kutoka kwetu," alisema Gumbo.
Alisema kuwa kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya kabla ya kuanza kwa msimu walipokuwa kambini Zanzibar ndio itakuwa silaha yao ya ushindi.
Hata hivyo, Gumbo amewataka wachezaji wenzake kujituma kwa moyo mmoja na kushirikina kwa pamoja.
|
|
?Phiri aikata maini Yanga |
|
Thursday, 05 August 2010 04:45 |
|
Na Mussa Soraga, Zanzibar
KAULI ya iliyotolewa na Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Patrick Phiri siku mbili baada ya kuanza kukinoa kikosi chake, ni sawa na kuikata maini watani wao wa jadi Yanga.
Yanga ambao wapo katika maandalizi makali chini ya Kostadin Papic 'Clinton' kwa lengo la kutaka kurudisha taji lao lililokwenda Msimbazi msimu uliopita, lakini kwa kauli ya Phiri wafute ndoto hizo.
Mara baada ya Phiri kukinoa kikosi hicho kwa siku mbili ameibuka na kusema kuwa 'hakuna mbabe katika Ligi Kuu Bara zaidi ya Simba'.
Phiri alitoa kauli hiyo juzi baada ya kumaliza mazoezi huku akiwa amezongwa na mashabiki lukuki ambao walitaka kumsikia kauli yake mara baada ya kuwasili kuinoa tena mabingwa hao.
|
|
Read more...
|
|
|
|
|
|
|
Page 6 of 52 |
Who's Online
We have 4 guests online
Powered by Business Times Ltd
Valid XHTML and CSS.