Sunday 05th of September 2010
Home
Habari za Michezo
|
Huwezi kufanikiwa bila vikwazo |
|
Saturday, 29 May 2010 16:41 |
|
MAISHA ni safari ndefu kama wengi wanavyosema, ndani ya safari hiyo huwezi kujua nini kitatokea mbele yako.
Lakini huwezi kuacha kusafiri, jambo hilo haliwezekani kwa kuwa ukishakuwa duniani tu wewe unakuwa ndani ya safari hiyo ya kimaisha.
Katika hili, watu wengi huogopa kwa kuwa hufikiria zaidi yatakayoweza kuwakuta ndani ya safari hiyo hasa vikwazo mbalimbali vitakavyo wakwamisha kufika kule wanapopataka.
Lakini ni muhimu kufahamu kuwa kila mtu hukumbana na vikwazo katika maisha, na vikwazo hivyo ndivyo ambavyo hutumiwa kwa ajili ya kuleta mafanikio.
|
|
Read more...
|
|
|
JINSI YA KUPATA MAPENZI UYATAKAYO KATIKA NDOA |
|
Saturday, 29 May 2010 16:39 |
|
KILA ndoa ina matatizo, na yanaweza kufumuka wakati wowote. La muhimu ni kwamba unapokuwa umeamua kujiingiza katika maisha ya ndoa unapaswa kujifunza jinsi ya kukabiliana na matatizo hayo ili yaweze kuisha salama na ndoa kuendelea kuwa salama.
Bila kujali umeenda umbali gani katika barabara hii ya ndoa, zipo kanuni rahisi lakini za muhimu za usalama katika barabara hii. Si rahisi sana kuzitekeleza kanuni hizi, kwa wanandoa walio wengi, lakini ni lazima kuzitekeleza iwapo wahusika wanapenda ndoa yao iwe salama.
Iwapo utazingatia kanuni hizi, utaifanya ndoa yako kuwa imara zaidi. Katika usalama huu utapata pia marupurupu – furaha, ngono, kuaminiana (kuaminiwa), mapenzi moto moto na kadhalika. Hebu sasa na tuziangalie kanuni zenyewe: -
|
|
Read more...
|
|
Thursday, 27 May 2010 15:17 |
|
Na Mwandishi Wetu
KIKOSI cha timu ya soka ya Simba, msimu ujao kitakuwa kipya kabisa baada ya kubomolewa na kusajili wachezaji wengine ambao wataleta mabadiliko katika kikosi hicho.
Simba ambao walipata mafanikio makubwa katika msimu wa mwaka 2003 ambapo walifanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuitupa nje timu ya Zamalek ya Misri.
Tangu msimu huo Simba haikufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake kiasi cha kushindwa kufanya makubwa ambayo waliyafanya katika kipindi hicho zaidi ya miaka saba sasa.
|
|
Read more...
|
|
|
Lindi waivua ubingwa Ilala |
|
Thursday, 27 May 2010 15:19 |
|
Na Erasto Stanslaus
TIMU ya mkoa wa Lindi 'Ilulu Stars' jana ilifanikiwa kuwavua ubingwa mabingwa watetezi wa michuano ya kombe la Taifa baada ya kuichapa mabao 3-0.
Matokeo hayo ya mchezo wa pili wa nusu fainali ya michuano hiyo uliochezwa katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam umeipeleka Lindi katika fainali itakayopigwa keshokutwa katika uwanja wa huo huo.
Lindi sasa itaivaa na timu ya mkoa wa Singida katika fainali wakati Ilala watakutana na Arusha katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu kesho.
|
|
Read more...
|
|
Thursday, 27 May 2010 15:15 |
|
Na Erasto Stanslaus
BAADA ya kuondokewa na mshambuliaji wake mahiri, Mrisho Ngassa klabu ya Yanga ipo mbioni kuondokewa na pacha wa mshambuliaji huyo, Jerry Tegete anayewaniwa na klabu ya Simba.
Kwa mujibu wa kiongozi mmoja anayeshughulikia mambo ya usajili wa klabu ya Simba, ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema wapo katika mazungumzo ya awali kumnasa mchezaji huyo.
|
|
Read more...
|
|
|
|
|
|
|
Page 42 of 52 |
Who's Online
We have 5 guests online
Powered by Business Times Ltd
Valid XHTML and CSS.