Sunday 05th of September 2010

Home
Habari za Michezo
Rooney amsononesha Ferguson
Monday, 23 August 2010 05:42

LONDON, Uingereza

ALEX Ferguson, amedai kuwa hajui Wayne Rooney, atamaliza lini ukame wa magoli. Takwimu zinaonesha, nyota hoyu wa Manchester United, hajafunga kwa dakika 1,076 katika timu yake na timu ya taifa.

Hilo linafufua ya msimu wa  2005/6 baada ya kucheza dakika 1,002 bila bao.Goli lake la mwisho alifunga Machi dhidi ya Bayern Munich nchini Ujerumani.

Fergie alisema jambo hilo, linaweza kumuumiza Rooney, ingawa anafurahishwa na kiwango chake sasa.Kocha huyo wa United alisema "nasema hili kila mara, mshambuliaji anahitaji kufunga, asipofunga anahisi hatafunga tena."Wayne, hana tofauti na washambuliaji wengine, ni watu wanaotaka kufanya jambo moja kwa moja."Ferguson, hata hivyo anaamini magoli yataanza kupatikana tena kutoka kwa nyota huyo.

Alipoulizwa kama Rooney amekuwa na woga, alisema "hilo ni jambo la kwaida kwa mshambuliaji yeyote Wayne hana tofauti na wengi.  "Wanataka kufunga na wakishindwa, wanahisi haitatokea tena".

 

 
Liverpool: Mascherano haondoki
Monday, 23 August 2010 05:40

LONDON, Uingereza

ROY Hodgson, juzi usiku alisema Inter Milan, imejiondoa katika mbio za kumtaka Javier Mascherano.

Hilo linamfanya nyota huyo wa Argentina, kubakiwa na miezi sita Anfield.

Mascherano, amekuwa akitaka kuondoka Liverpool, kwa kuwa mke wake hafurahii maisha ya  England, huku kocha wake wa zamani Rafa Benitez, akimtaka Serie A ya Italia.

Kocha huyo wa Inter Milan,   Benitez, anamtaka Dirk Kuyt, lakini Hodgson, amedai alizungumza na Rais wa Milan, Massimo Moratti, na kumuahidi hatasaini mchezaji yeyote wa Anfield.

 
Balotelli: Mimi si mtukutu
Thursday, 19 August 2010 06:02

MANCHESTER, Uingereza

BAADA ya Jose Mourinho, kudai Mario Balotelli, haongozeki na hana akili, mchezaji huyo amedai yeye si mtukutu kama inavyodhaniwa. 

Nyota huyo aliyesajiliwa na Manchester City, amekuwa  akishutumiwa kutokana na utukutu wake hasa alipokuwa Inter Milan chini ya kocha aliyehamia Real Madrid, Jose Mourinho.

Baada ya kujiunga na kocha Roberto Mancini, kwa pauni milioni 22.5, nyota huyo alimwambia kocha wake kuwa hana haja ya kuwa na wasiwasi naye.

Read more...
 
Wananikera
Thursday, 19 August 2010 06:05

*Ferguson aibwatukia Man City

MANCHESTER, Uingereza

KOCHA wa Manchester United, Alex  Ferguson, ameibwatukia Manchester City kwa kitendo chao cha kusaini wachezaji kwa gharama kubwa.

Fergie, amekerwa na kitendo cha timu hiyo kumsaini, James Milner, kwa pauni milioni 24 kutoka Aston Villa jana, na kumfanya kocha wa Man City, Roberto Mancini kutumia kiasi cha pauni milioni 130 hadi sasa.

Timu hiyo pia, ilitumia kiasi cha pauni milioni 22.5 kumsaini, Mario Balotelli, kutoka Inter Milan, na kumfanya mmiliki wa timu hiyo Bilionea wa Saud Arabia, Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan, kutumia kiasi cha pauni milioni 325, tangu alipoichukua timu hiyo miaka miwili iliyopita.

Read more...
 
Menezes: Neymar itose Chelsea
Thursday, 19 August 2010 05:41

 

KOCHA MKuu mpya wa Brazil, Mano Menezes amemuonya kiungo mshambuliaji mpya wa kikosi chake, Neymar, juu ya kujiunga na klabu ya Chelsea na kusema kuwa kinda huyo anatakiwa kuendelea kujifunza akiwa Santos.

Neymar ambaye ni mara yake ya kwanza kujiunga na timu ya taifa ya Brazil, ametoka katika klabu ambayo ndiyo iliyomkuza nyota wa zamani wa Brazil, Pele.

Inaaminika kuwa, Chelsea, imeshindwa kwa pauni milioni 24 katika ofa ya mshambuliaji huyo ambaye alifunga goli kwa mara ya kwanza juzi akiwa na Brazil.

Read more...
 
« StartPrev12345678910NextEnd »

Page 5 of 52

Swali la Leo

"Kitendo cha mabondia wa ngumi za ridhaa kususia mashindano kutokana na kutopatiwa chakura na nauli, ni maamuzi sahihi kwa maslahi ya Taifa letu?"
 

Who's Online

We have 3 guests online

Login Form




Powered by Business Times Ltd Valid XHTML and CSS.