Sunday 05th of September 2010

Home
Habari za Michezo
Yanga wala hasara tena
Thursday, 26 August 2010 05:39

Na Erasto Stanslaus

TIMU ya Yanga imepata balaa lingine kwa kumkosa mshambuliaji wake Mghana Keneth Asamoah katika michezo yake kadhaa ya Ligi Kuu Bara bila kupata matumaini ya lini wanaweza kumtumia.

Yanga ambao walikuwa na matumaini makubwa na mshambuliaji huyo ambaye alianza kwa kasi katika upachikaji wa mabao katika michezo kadhaa aliyoichezea timu hiyo.

Asamoah alikuwa gumzo kwa wapenzi wa soka nchini baada ya kuifungia timu yake mabao matano katika michezo minne aliyoichezea timu hiyo huku katika mchezo mmoja akifunga mabao 3.

Read more...
 
Ochan hana tatizo la saikolojia - Mziray
Thursday, 26 August 2010 05:38

Na Julius Kihampa
MTAALAM wa saikolojia wa Simba, Syllersaid Mziray amesema mshambuliaji wao mpya kutoka Uganda, Patrick Ochan hakuwa na tatizo la kisaikolojia kama ambavyo wengi wanadhani.

Ochan ambaye ndiye mchezaji pekee aliyesajiliwa katika klabu hiyo kwa pesa nyingi, bado hajaonesha kiwango kikubwa kama ilivyotarajiwa na wapenzi wa timu hiyo tangu kuwasili kwake.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili juzi jijini Dar es Salaam, Mziray alisema mchezaji huyo anataka utulivu wa muda ili kuweza kuendana na kasi ya Simba na soka la Tanzania kwa ujumla.

Alisema uongozi wa Simba ulimsajili mchezaji huyo kwa makusudi na inatambua uwezo wake hivyo ni tatizo ambalo hakuwanalo wakati akihitajiwa kukipiga katika kikosi cha mabingwa hao wa Bara.

"Hana tatizo lolote la kisaikolojia ama vinginevyo, ni tatizo ambalo mtu ama mchezaji yeyote angeweza kuwa nalo tu," alisema Mziray.

 
Fergie aiunga mkono England
Thursday, 26 August 2010 05:32

MANCHESTER, England

KOCHA nguli wa Manchester United, Mscostland, Alex Ferguson ameiunga mkono England kuandaa Fainali za Kombe la Dunia 2018.

Meneja huyo wa Man United, aliishauri FIFA kuipa nafasi England, walipofanya ziara katika uwanja wa Old Trafford.

Fergie alisema: "Hiyo itakuwa nafasi kwa wachezaji na mashabiki wa England kutoka katika viwanja vya mazoezi hadi kwenye mechi za Kombe la Dunia.

"Na kutokana na uungwana wa watu wa England kila mtu atajisikia kukaribishwa katika ardhi ya nchi hii."

FIFA wapo nchini England kwa lengo la kukagua viwanja vitakavyoweza kutumika katika fainali hizo lakini jibu la mwisho watatangaza Desemba. England inachuana na Russia kuwania nafasi hiyo.

 

 
Capello kuibomoa England
Thursday, 26 August 2010 05:33

LONDON, England

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya England, Fabio Capello anafikiria kukibomoa kikosi chake na kukiunda upya, akitumia wachezaji chipukizi zaidi.

Capello anatarajia kuunda kikosi ambacho kitakuwa na wachezaji wengi vijana wanaounda kikosi cha vijana chini ya miaka 21 cha timu hiyo.

Kocha huyo aliyeiongoza Three Lions katika fainali za kombe la Dunia anatarajia kuunda kikosi hicho katika maandalizi ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Mataifa Ulaya.

Mpango wa Capello kukibomoa kikosi hicho umekuja baada ya kumaliza mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Hungury uliochezwa wiki mbili zilizopita.

Read more...
 
Simba yaanza kishindo.
Monday, 23 August 2010 06:02

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la pili dhidi ya African Lyon Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana. Simba ilishinda mabao 2-0.(Picha na Zuberi Mussa

 
« StartPrev12345678910NextEnd »

Page 3 of 52

Swali la Leo

"Kitendo cha mabondia wa ngumi za ridhaa kususia mashindano kutokana na kutopatiwa chakura na nauli, ni maamuzi sahihi kwa maslahi ya Taifa letu?"
 

Who's Online

We have 7 guests online

Login Form




Powered by Business Times Ltd Valid XHTML and CSS.