BREAKING NEWS: Manara atimuliwa rasmi Simba

1 month ago 590

BREAKING:OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amebwaga manyanga ndani ya Simba na kwa sasa nafasi yake inachukuliwa na Ezekiel Kamwaga ambaye anakuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu kwa kipindi cha miezi miwili.

Taarifa rasmi ambayo imetolewa na Simba kupitia ukurasa wao wa Instagram imeeleza kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, kwa kauli moja imeridhia matakwa ya ndugu Haji Manara ya kutoendelea kuhudumu katika nafasi ya msemaji wa Klabu ya Simba.


Bodi inamshukuru kwa maneno aliyoyatumia kuwaaga wana Simba katika kundi la viongozi wa Simba, (Simba HQ)  na kwa kazi aliyoifanyia Klabu ya Simba katika kipindi alichoshika nafasi hiyo na inamtakia heri katika shughuli zake.